FUJO ZA NYETI ZAMPELEKA JELA SEMANDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Mtu mmoja Sendama Mabula (24), Mkazi wa Sambaru, Kata ya Mang’onyi, Tarafa na Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida amehukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya fujo akidai kuibiwa nyeti zake.

Hukumu hiyo imetolewa Aprili 10, 2026 na Mahakama mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mwanzo Ikungi baada ya ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo kujitosheleza.

Awali Aprili 9, 2026 Mshitakiwa akiwa katika Kijiji cha Sambar, Kata ya Mang’onyi, Tarafa na Wilaya ya Ikungi aliwafanyia fujo na vurugu Richard Michael Isango (38), Mkurugenzi wa Kampuni ya ulinzi ya GSY Services and Security Company na Shabani Abdallah Shabani, (32).

Wengine ni Msimamizi wa GSY Services and Security Company wote wakazi wa Singida Mjini akiwatuhumu kuiba sehemu zake za siri ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa Mahakamani Aprili 10, 2026 na kuhukumiwa siku hiyo.

Hakimu mkazi Mbangula amesema kuwa ametoa adhabu kwa Mshitakiwa ili iwe funzo kwake na kwa jamii kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *