
Wawekezaji Katika Sekta Ya Mawasiliano Hususani Wamiliki Wa Vyombo Vya Habari Wametakiwa Kuzingatia Masharti Ya Leseni Zao Na Kufikisha Huduma Katika Maeneo Yote Waliyoomba Kutoa Huduma.
Ushauri Huo Umetolewa Na Meneja Wa Mamlaka Ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda Ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo Wakati Akitoa Mada Katika Semina Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Shinyanga Ambapo Pia Ametoa Wito Kwa Wenye Uhitaji Wa Kuanzisha Vyombo Vya Habari Kuwatumia Wataalam Wa Mamlaka Hiyo Ili Kupata Msaada Wa Ushauri Juu Ya Namna Ya Kufuata Taratibu Za Usajili.
Aidha Amevitaka Vyombo Vya Habari Kuwa Na Ushindani Wenye Tija Badala Ya Kuwa Na Ushindani Unaosababisha Mizozo Na Migogoro Miongoni Mwa Vyombo Vya Habari Vinavyohudumia Wananchi.
Kupitia Semina Hiyo,Mwezeshaji Na Mwenyekiti Wa Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Mwanza Edwin Soko Amewataka Waandishi Wa Habari Kuzingatia Sheria,Kanuni Na Taratibu Za Uandishi Kutokana Na Unyeti Wa Sekta Ya Habari Na Kuelezea Baadhi Ya Matakwa Ya Kisheria.
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Shinyanga Greyson Kakuru Amesema Anaamini Mafunzo Hayo Ni Muhimu Kwa Waandishi Wa Habari Kwa kuwa Yamewakumbusha Kuhusiana Na Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati Wa Utekelezaji Wa Majukumu Yao Ya Kila Siku.