Fountain Gate yainunua Gwambina Complex Mwanza

Taasisi ya Fountain Gate Sports, imeununua uwanja wa Gwambina Complex uliopo wiliyani Misungwi jijini Mwanza, ambao ulikuwa ukitumiwa na timu ya Gwambina FC na sasa uwanja huo utatambulika kwa jina la Fountain Gate Stadium Mwanza.

Hii ni hatua nyingine kubwa kwa taasisi hiyo yenye makao makuu yake jijini Dodoma, baada ya katikati mwa mwaka huu kutangaza kuinunua klabu ya Singida Big Stars ya mkoani Singida na kuiita Singida Fountain Gate FC.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Fountain Gate Sports, Calvin Shaban Herry, amesema dhumuni la kuuchukua uwanja huo ni kuendeleza programu mbalimbali za vijana wa kike na kiume kutoka Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Pamoja na kuuchukua uwanja huo, taasisi hiyo pia imeichukua na shule ya sekondari Elpas iliyopo wilayani hapo na sasa itakuwa chini ya Fountain Gate Schools.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *