Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Flaviana Matata Foundation yaunga mkono serikali mkoani Shinyanga kuboresha mazingira ya mtoto wa kike shuleni

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamiringi Macha amepongeza jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation katika kuhakikisha mazingira bora ya wanafunzi wakike kwa kuwajengea vyumba vya kujisitiri pindi wanapokuwa katika siku zao za hedhi mashuleni.

RC Macha ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyoo vyenye matundu 12 pamoja na vyumba viwili kimoja kikiwa kwa ajili ya kijistiri na kingie cha Watoto wenye mahitaji maalum yaani walemavu katika Shule ya Sekondari Masekelo iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

“Niipongeze Taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kujenga mradi huu kwani utawasaidia wanafunzi wa shule hii ya Masekelo hususani wasichana kujisitiri na kuwa na faragha hivyo kupata utulivu wa akili pindi wanapokuwa shuleni, na niziombe Taasisi na Mashirika mengine kushirikiana na kuunga mkono jitihada za Serikali ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na mazingira bora, rafiki na waweze kusoma kwa uhuru zaidi” amesema RC Macha.

Kwa upande wake Muanzilishi wa Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Flaviana Matata Foundation Bi. Flaviana Matata ameishukuru Serikali kwa kuthamini jitihada wanazofanya na ameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika shughuli za kuisaidia jamii kwani anajisikia fahari kuwasaidia watoto wa kike wanaotokea kwenye mazingira magumu huku akisisitiza kuwa Taasisi yake inajihusisha pia na utoaji wa elimu ya uzazi salama, pamoja na kuzuia mimba za utotoni kwa kutoa elimu ya uzazi.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Masekelo Mwl. Vicent Kanyogoto amesema kuwa Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 kwa fedha za Serikali Kuu ina changamoto ya walimu ambapo mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 988 na walimu 23 ambao hawaendani na idadi ya wanafunzi iliyopo hususan kwa masomo ya Sayansi.

Flaviana Matata Foundation inafadhili jumla ya shule 10 mkoani Shinyanga ambapo Masekelo Sekondari ni moja kati ya shule hizo na taasisi hiyo inahudumia wanafunzi wa kike takribani 408 kwa kufadhili gharama za masomo hasa kwa wanaotoka katika mazingira magumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *