Staa wa filamu kutoka nchini Marekani, Will Smith ametangaza rasmi ujio wa Filamu ya “Bad Boys 4” ambayo itatoka Juni 7, 2024.

Will Smith ametioa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Filamu ya mwisho ya Bad Boys ilitoka Mwaka 2020 na kufanikiwa kuingiza zaidi ya Tsh. Bilioni 996.7 kupitia Sinema.
‘Bad Boys III’ iliwakutanisha Smith na Lawrence miaka 20 baada ya Bad Boys II.


