Fidla ya Stradivari (Violin) yenye umri wa miaka 311 imeuzwa kwa $11.25 milioni huko Sotheby’s siku ya Ijumaa, katika mnada ambao uliotazamwa kwa karibu na uliovutia Wawekezaji na Wanamuziki wa zamani.
Fidla hiyo, ilitengenezwa na Mwanaluthier mashuhuri wa Kiitaliano, Antonio Stradivari mwaka 1714, wakati wa kile kinachoitwa kipindi cha dhahabu cha utengenezaji wa Violin.

Baadaye, ilimilikiwa na mmoja wa wapiga Violin wakubwa wa karne ya 19 mzaliwa wa Hungaria, Joseph Joachim ambaye alikuwa ni mshiriki wa karibu wa Johannes Brahms.
Stradivari iliuzwa na Conservatory ya New England, ambayo inapanga kutumia mapato ya mauzo hayo kuweka mpango wa ufadhili wa wanafunzi na hapo awali Violin hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mhitimu wa shule hiyo, Si-Hon Ma, aliyefariki mwaka wa 2009.

Baadaye, chombo hicho cha Conservatory ya New England mwaka wa 2015 kilitolewa kwa masharti kwamba kinaweza kuuzwa siku yoyote, ili kufadhili masomo ya Wanafunzi.
Rais wa Chuo hicho, Andrea Kalyn alisema “Sasa tunayo nafasi ya kunufaisha wanafunzi wengi zaidi – vizazi vya Wanafunzi vijavyo.”
