Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum na Mudathir Yahya wa Yanga wamepigwa faini ya Tsh milioni mbili kila mmoja kwa kosa la kutegea kuingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo wao hadi zoezi la kupeana mikono lilipomalizika .

Wengine ni Habibu Kyombo wa Singida Fountaine Gate ametozwa faini ya Milioni moja kwa kosa la kufanya kitu kama Imani za kishirikina katika mchezo namba 46 ambao walicheza na Namungo. Pia Klabu ya Singida FG imetozwa faini ya Milioni mbili kwa kosa walilofanya kwenye mchezo Namba 50 dhidi ya Yanga, ambapo waligomea kutumia vumba maalumu vya kuvalia nguo.
