Familia ya Gcaba yakanusha kuhusika na mauaji ya AKA na Tibs

Familia ya Gcaba imeeleza kuwa taarifa iliyotolewa na waendesha mashtaka inayomhusisha mfanyabiashara Sydney Mfundo Gcaba kuwa mhusika wa mauaji ya mwanamuziki maarufu AKA na Tebello “Tibz” Motsoane sio kweli

Katika taarifa hayo, iliyotolewa siku ya Jumapili, Mandla Gcaba alisema Mfundo Gcaba, ambaye alitajwa kuwa mtu aliyeweka R800,000 (Tsh.Milioni 109) kwenye akaunti ya benki ya Mziwethemba Gwabeni, siku moja baada ya AKA kuuawa alikuwa kwa ajili ya biashara.

Mnamo Februari 10, 2023, nje ya mkahawa huko Durban, kwenye pwani ya mashariki ya Afrika Kusini, AKA (jina halisi la Kiernan Forbes) na Tebello “Tibz” Motsoane walipigwa risasi na kuuawa. Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha sana kwa watu wengi wa Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *