Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewazawadia zawadi maalum Simba SC, kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex kwa ajili ya mchezo wa
fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mchezo huo unatarajia kufanyika Mei 25, 2025 na Rais Dkt. Mwinyi analenga kudhihirisha mapenzi yake ya dhati katika michezo pamoja na kuhamasisha ushindi kwa timu ya Simba SC dhidi ya RS Berkane ya
Morocco.
