Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Faida za kula Mihogo mibichi kwa mwanaume

Ukikuta mwanamama au kijana anatembeza mihogo (mibichi) na nazi mbata barabarani kama wewe mwanaume basi nunua kwani zina faida kubwa sana kwenu na vinauwezo mkubwa wa kurejesha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.

Uwezo wa mihogo na nazi mbata au kwa kuchanganya na karanga katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata au karanga.

Mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) na karanga ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuimarisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana kwenye vyakula hivyo. Zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi, karanga na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho. Mihogo mibichi, karanga na nazi mbata husaidia kuimarisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.

Faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi au karanga aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho ‘lauric acid’.


Hizi ni chache tu unaweza kuongeza faida zingine kiafya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *