EWURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta, zitakazoanza kutumika hii leo Septemba 2, 2026.

Taarifa ya EWURA imeeleza kuwa, Septemba 2026 bei za Mafuta nchini zimeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita na Petrol na Shilingi 101 kwa lita ya Dizeli, kutokana na hatua mbalimbali ambazo Serikali imezichukua.

Kwa Dar es Salaam, bei ya rejareja kwa lita moja itakuwa Tsh 3,796 kwa petroli, Tsh 3,877 kwa Dizeli na Tsh 3,713 kwa mafuta ya taa.

Aidha, EWURA imewataka Wafanyabiashara wa Mafuta kuuza bidhaa hizo kwa bei zisizozidi viwango vilivyotangazwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *