Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za Mafuta ya Petroli, Dizeli, na Taa, zitakazotumika kuanzia hii leo Agosti 5, 2026.
Bei ya Lita ya Dizeli imeshuka kwa Shilingi 204 huku Lita Petroli ikishuka kwa Shilingi na Mafuta ya Taa yakishuka kwa Shilingi 440.
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, bei kikomo za rejareja ni Tsh 3,898 kwa Lita ya Petroli, Tsh 3,978 kwa Dizeli na Sh 4,003 kwa Mafuta ya taa.









