Najua wadada wengi wanakuwa na pochi ama handbag kwa kiingereza, ila je unaweka vitu gani kwenye pochi yako unayobebba?
Leo nitakujuza vitu vinne muhimu vya kuweka kwenye pochi yako iliusidhalilike endapo litatokea lolote.
Moja, hakikisha pochi yako haikosi pesa taslimu au ATM Card… hizi zitasaidia wewe labda kufanya malipo ya kitu au manunuzi. Mfano uanataka kula kwenye mgahawa unaweza lipia cash au kwa Card.
Mbili.. hivi ni vingi ila ndio muhimu hapa hakikisha una wipes/tissue (Tishu), perfume (chupa ndogo/min perfume) Lip shine/lipbam, pedi, Sunscren (Hii inalinda Ngozi yako ni kama mafuta yani), Kitakasa mikono.
Simu na Chaji… kutokuwa hewani kwa Maisha ya sasa ni kosa kubwa unaweza kupitwa na jambo la msingi hivyo kwa gharama yoyote unatakiwa kuwa hewani.
Kitambulisho cha sura yako (ID) hii itakuwaokoa endapo kumetoka kitu watu kukutambua kwa haraka hapa unaweza kuwa na NIDA, Kitambulisho cha kazi, Leseni ya udereve n.k