Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na wadau wa CIHEB-TZ, imeendesha mafunzo ya kujenga uwezo kwa Kamati ya Uokoaji Ngazi ya Mkoa wa Mwanza, Emergency Response Team – ERT.
Kikao hicho, kililenga kujadili matokeo ya tathmini ya uendeshaji wa vituo vya uratibu wa operesheni za dharura na maafa, ikiwemo Kituo cha Sekta Jumuishi – EOCC na Kituo cha Dharura za Afya ya Jamii – PHEOOC.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Daniel Machunda amesema awali masuala ya usimamizi wa maafa hayakuwa yakipewa uzito unaostahili, lakini sasa Serikali imeyafanya kuwa kipaumbele katika kulinda maisha na mali za wananchi.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Mwanza utaendelea kuimarisha maandalizi, ufuatiliaji wa vihatarishi na kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na maafa.

Washiriki wamekubaliana kutoa kipaumbele katika mafunzo endelevu, kuimarisha usimamizi wa takwimu na nyaraka.



