Erick Mwijage atimkia FC West Armenia

Mchezaji Erick Mwijage wa kikosi cha Kagera Sugar FC, ametimkia katika klabu ya FC West Armenia inayoshiriki ligi kuu nchini Armenia kama mchezaji huru, baada ya mkataba wake na Kagera Sugar FC kufikia tamati.

Mwijage ni mchezaji aliyeibuka katika timu ya vijana ya Kagera Sugar FC kabla ya kung’aa vema katika takribani misimu yake mitatu ya kuitumia timu ya kubwa.

FC West Armenia ni timu iliyopanda ligi kuu nchini Armenia msimu huu. Kama itakumbukwa hivi karibuni timu hiyo iliisaini makubaliano na Simba SC ya kutoa fursa kwa kuuziana wachezaji, maendeleo ya ufundi, soka la vijana na maendeleo ya soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *