ENDELEENI KUTOA ELIMU YA UTAPELI MTANDAONI – SILAA

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameyaelekeza makampuni ya simu nchini kuendeleza kampeni ya kutoa elimu kwa watumiaji wa simu na kuongeza umakini kwenye matumizi ya simu na wao kama Serikali wataendelea kuhakikisha wanapunguza utapeli unaofanyika.

Waziri Silaa ametoa maelekezo hayo  leo Januari 31,2025 Bungeni hapa Jijini Dodoma wakati akitokoa ufafanuzi juu ya ongezeko la utapaleni nchini huku akiongeza kuwa jeshi la polisi kupiitia Wizara ya Mambo ya Ndani litafanya oparesheni hasa katika mikoa ya Rukwa na Morogoro ambayo kwenye takwimu za utapeli wa mtandao inaongoza nchini.

Aidha akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angeline Mabula aliyetaka kujua kama Serikali haioni kuwa inawajengea mazingira magumu viongozi ambao majina yao yanatumika kutapeli wananchi Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amsema Serikali itahakikisha haiweki mazingira magumu ya kuona kwamba jamii inaendelea kutapeliwa kwani wao kazi yao kubwa ni kuhakikisha jamii inapata maendeleo na mazingira rafiki na kila mmoja anakuwa salama anapotumia laini ya mtandao wa simu.

“Taarifa zote mnazotupatia hata juzi tu hapa nimepokea karibia wabunge watatu wote wananijia na vidhibitisho majina ya baadhi ya viongozi yanavyoendelea kutumika, tayari nimekwisha kuyaripoti TCRA na kazi kubwa sana inaendelea kufanyika na suala la mrejesho wa nini kimefanyika tutaendelea kusisitizana na watendaji kuona kwamba wewe uliyeleta taarifa yako basi uweze kupata mrejesho uwe ni kiongozi au mwananchi wa kawaida,”amesema.

Naye Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson amekili kuwa tatizo hilo ni kubwa na watu wanatapeliwa kupitia jina lake mpaka amechoka kutoa taarifa kwani ripoti anatoa lakini bado unaendelea.

“Na haya matangazo yao hayawekwi kifichoni watu wanatangazi sijui kwenye mitandao ile ya kijamii Facebook kuna matangazo, Instagram kuna matangazo huko kote wanatangaza na wapo wameweka namba za simu, wanapigia watu simu na sasa hivi kuna ile akili mnemba mtu anasema umenipigia wewe simu na anaongea nawewe sasa mimi Spika naweza kumpigia simu mwananchi kwamba nakopesha hela lakini ndiyo hivo watu wanatapeliwa kila siku,”amesema.

Amesema kama ni juhudi basi jambo hilo limekuwa kubwa nchini kwasababu kwingine wanakosafiri hawasikii mambo hayo na kuhoji kuwa ni kwanini watanzania wanatapeliwa kiasi hicho na wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ipo na kama shida ni wao iko wapi ili waifanyie kazi maana umezidi hasa wa jina lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *