ENDAMAGHAAY WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI BABATI, BILIONI 1.9 ZATUMIKA

Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wananchi zaidi ya 5,000 kutoka vijiji vitatu Endamaghaay, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, wameanza kunufaika na mradi wa maji safi na salama ulitekelezwa na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), uliolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilion 1.9.

Mradi huo umewekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mabio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda ambaye ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo uliohahakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji na kupunguza adha ya kubeba maji umbali mrefu.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara Mhandisi James Kionaomela, amesema mradi huo unahusisha tanki la kuhifadhi maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 na utawawezesha wananchi kuunganishiwa huduma ya maji moja kwa moja majumbani, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa maji kwa jamii.

Aidha, Baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo wameishukuru Serikali kwa utekelezaji wake, wakisema utapunguza umbali wa kufuata maji, kuokoa muda Pamoja na kuongeza fursa za kufanya shughuli za maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *