Elimu ya lazima siyo miaka 7 tena ni miaka 10

Serikali imefanya maboresho kwenye baadhi ya maeneo katika sera ya elimu na mafunzo ili kutoa elimu ya ujuzi badala ya elimu ya taaluma pekee ambapo elimu ya lazima itakuwa ya miaka 10 badala ya saba kama ilivyo sasa.

Akitoa taarifa kuhusu maboresho hayo leo November 02,2023 Bungeni Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa maboresho hayo utaanza mwaka 2027 sambamba na kufuta mtihani wa darasa la saba na badala yake kuanza kufanyika kwa tathmini darasa la sita kwa ajili ya kujiunga na elimu ya lazima ya sekondari.

Aidha amesema kuwa maboresho ya sera hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kuhusu mapitio ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mitaala ya elimu katika ngazi mbalimbali ili ijikite katika kutoa elimu ya ujuzi baadala ya elimu ya taaluma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *