Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji Makambako, Rashid Mustapha Makocha amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 10,000.
Akisoma hukumu katika kesi hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Isaac Mlowe amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa Pamoja na kosa la kumshawishi mkulima ili aweze kumsajili kwenye daftari la wakulima ili awe mnufaika wa mbolea ya ruzuku iliyotolewa na serikali.
Mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kutumikia kifungo cha Miaka 5 jela kwa kosa la Kwanza na Faini ya Tsh. 500,000 au kifungo cha Miaka 5 kwa kosa la Pili. Pia, imeamuliwa Fedha ya mtego, (Tsh. 10,000) irudishwe Serikalini.