Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Dullah Mbabe kuzipiga tena na Katompa

Bondia tishio katika uzito wa Super Middleweight nchini Tanzania, Dullah Mbabe anatarajiwa kupanda ulingoni Novemba 25 mwaka huu, kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha, dhidi ya Mkongoman Tshimanga Katompa.

Hili ni pambano la marudiano baada ya lile la awali lililopigwa Oktoba 9 mwaka 2021 kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam, Dullah Mbabe kupoteza kwa pointi za majaji wote.

Pambano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Lady in Red Promotion chini ya Promota wake Mhe. Sofia Mwakagenda ambaye ni Mbunge wa viti maalum mkoani Mbeya, limebeba dhima ya utalii wa ndani likiitwa ‘BOXING WITH TOURISM’.

Mbali na pambano kuu la Dullah Mbabe na Tshimanga Katompa, mabondia wengine wakali kama Loren Japhet, Shaban Ndaro, Saleh Mkalekwa, Jacob Maganga na Sarah Alex wataupamba ulingo huo siku hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *