Rapa Drake na J. Cole wameamua kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwa kupiga picha ambayo magwiji hao wasoka walipiga kuelekea kombe la Dunia 2022. Ila wao wametumia katika video yao ya muziki ya ‘First Person Shooter’, iliyotoka Jumatano (Jana).

Drake na Cole wanatarajiwa kufanya tour ya pamoja ifikapo 2024 na tour hiyo itaitwa ‘All A Blur’ na itaanza Januari 18.
Picha ya CR7 na Messi ilipigwa na mpiga picha maarufu wa Marekani, Annie Leibovitz mwaka 2022 wakati wa Fainali za Kombe la Dunia, Qatar kama sehemu ya ushirikiano wao wa kulipwa na Louis Vuitton.
