DPP AONDOA SHAURI, DKT. SLAA AACHILIWA HURU

Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Dkt. Slaa alishtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, na leo Februari 27, 2025 wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi, Franco Kiswaga.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Balozi Willibrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkataba ya Bandari jijini Dar es Salaam jana.Picha na Sunday George

Wakili Mrema alieleza mahakamani hapo kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *