Don Jazzy atafuta wakuiokoa lebo yake

Katika makala iliyochapishwa na Billboard mnamo Oktoba 6, 2023, Mavin Records iko katika harakati za kupokea uwekezaji kutoka nje ya Nigeria ili kupata mauzo ya moja kwa moja.

Wakati huo inaelezwa kuwa thamani ya Mavin, ni kuanzia dola milioni 125 hadi 200, zaidi ya Bilioni 400 za Kitanzania na Makala ya Billboard ilibainisha kuwa kuna kampuni tofauti za uwekezaji zinaitaka lebo hiyo ikiwemo Universal Music Group (UMG) na HYBE.

Uwekezaji wa mwisho katika Mavin Records ulikuwa Januari 2019, ambapo ilipokea mamilioni ya dola kutoka kwenye kampuni ya Kupanda Holdings.

Mpaka sasa lebo hiyo inawasanii tishio kama Rema, Ayra Starr, Crayon, Bayanni na wengine lakini pia producers Jazzy mwenyewe, Altims, London, Baby Fresh na Andre Vibez.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *