
Afisa Afya Mkoa Dodoma, Nelson Rumbeli amesema kuwa mkoa wa Dodoma umejipanga vyema kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu endapo utatokea kutokana na mvua za mara kwa mara zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Rumbeli ameyabainisha hayo leo Desemba 12,2023 wakati akizungumza na Jambo FM kuhusiana na namna ambavyo mkoa umejipanga kukabiliana na ugonjwa huo endapo utatokea na kuongeza kuwa suala kubwa ambalo wanazingatia ni usafi.
Aidha amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanachemsha maji ya kunywa kwani yanaweza kuwa na bakteria wanao sababisha ugonjwa wa Kipindupindu.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2017, shirika la afya Duniani (WHO) lilipitisha mkakati wa kukabiliana na ugonjwa huo, uliolenga kupunguza vifo vitokanavyo na kipindupindu kwa asilimia 90% ifikapo mwaka 2030.