DODOMA WAHIMIZWA KUSAJILI ARDHI KUPATA HAKI MILIKI

Na Gideon Gregory  – Dodoma.

Kutokana na uwepo wa watu wengi wanaohamia Jijini Dodoma kwasasa, Mbunge wa Dodoma Mjini Pascal Chinyele amewahimiza wanachi kuhakikisha wanasajili ardhi zao, ili wapate haki miliki na kuondokana na migogoro ya ardhi. 

Chinyele ameyabainisha hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye ibada ya umoja wa Madhehebu ya Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Mkoa humo iliyofanyika Aprili 6,2026 katika uwanja wa Jamhuri. 

“Sasa hivi Jiji letu linaingiliwa na wageni, Watanzania wanahamia Dodoma kwa kiasi kikubwa sana, moja ya changamoto ambazo nimekuwa nikizipata kutoka kwa wananchi ni kudhurumiwa ardhi zao kwa namna moja au nyingine.

Wanatokea watu wanakuja na hati miliki na kuwatoa wakazi ambao wana nyaraka halali lakini inakuwa tu ni bahati mbaya hawana hati miliki, ndugu zangu nawaomba sana wale ambao mnamiliki ardhi na hamjatafuta hati miliki fuateni utaratibu mwende mkasajili ardhi zenu,” amesema. 

Amesema kwasasa Jiji linapoelekea linahamiwa na Watanzania wengi hivyo suala la ardhi ni muhimu, hususani wale wanaotoka katika maeneo ya pembezoni ambayo hayajapimwa ili wawe salama katika ardhi zao.

Akimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amewasihi waumini kutambua na kuishi katika nafasi zao.

“Mkristo wa leo lazima aendelee kukumbushwa kupitia salama, maombi, maubiri na makongamano kama haya, mkristo wa leo lazima afahamu nafasi yake katika jamii na mkristo wa leo lazima awe chanzo cha furaha na amani katika jamii,”amesema. 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Mch. Michael Peter amesema lengo na umoja huo ni kuunganisha mwili wa Kristo kwa pamoja na kufanya kuwa jukwaa la kiroho ambalo linawaleta waumini wote kwa pamoja na kujenga umoja katika Jiji la Dodoma. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *