Spika Dkt Tulia Ackson ameshinda na kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kwa kura 172 za Tanzania, huku Somalia wakipata kura 11, Senegal kura 59 na Malawi wakipata kura 61 katika Mkutano huo wa 147.
Uchaguzi huo umefanyika leo nchini Angola katika Jiji la Luanda na katika maelezo yake wakati akiomba kura jana, Dkt. Tulia aliwaahidi kusimamia misingi ya Umoja kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi.