DKT. SAMIA KUSHIRIKI SHEREHE ZA UAPISHO WA RAIS HICHILEMA ZAMBIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 1, 2026, ameondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Hakainde Hichilema.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika Agosti 13, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania
na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *