DKT. SAMIA AWAPA MATUMAINI WAKULIMA UNUNUZI MAHINDI

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kuangalia namna ya kuendelea kununua mahindi kwa wakulima kupitia Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Kauli hiyo ya Dkt Samia, inakuja baada ya takriban miezi minne tangu NFRA ilipoacha kununua mahindi kwa wakulima baada ya kumalizika kwa bajeti iliyokuwa imepangwa na Serikali kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha.

Dkt Samia ametoa maelekezo hayo leo, Jumapili Oktoba 19, 2025 alipozungumza na wananchi wa Sumbawanga mkoani Rukwa, katika mkutano wake wa kampeni za urais, zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Ingawa bajeti ilishaisha, amemtaka Dk Mwigulu kwenda kuangalia uwezekano wa kupatikana kwa fedha, ili Serikali iendelee kununua mahindi kwa wakulima.

Ameeleza wananchi wameendelea kuwa na mazao hayo, kwa kuwa Serikali iliwapa ruzuku ya mbolea iliyosababisha uzalishaji uongezeke.

“Niwaombe kapekueni muone uwezekano, tuendelee kununua mahindi kwa wakulima,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *