DKT. SAMIA ATANGAZA NEEMA, ZIWA BABATI KUKUZA UCHUMI WA MANYARA

Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga fedha ya kununua Mitambo ya kuondoa Magugu katika maziwa Nchini, likiwemo ziwa Babati.

Dkt. Samia ameyasema hayo hii leo wakati akihitimisha kampeini mkoani Manyara, zilizofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani, akisema lengo ni kuhakikisha maziwa yote yanakuwa masafi na kuanza kutumika katika shughuli ya Uvuvi na Utalii.

Amesema, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Kwa miaka miatano ijayo atanunua boti katika mkoa wa Manyara ikiwemo boti ya usalama na boti tatu zitasaidia katika shughuli za uvuvi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima amesema wanatarajia kushinda Kwa kishindo katika kata zote 142 zilizopo Mkoani Manyara, kutokana na kazi kubwa ya kukuza uchumi wa Taifa ambayo imefanywa na Dkt. Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *