Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake katika miaka mitano ijayo, inatarajia kukamilisha ujenzi wa mradi wa soko la samaki wilayani Pangani mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Dkt Samia, soko hilo la kimataifa litajengwa katika Kata ya Kipungwi na kwamba tayari hatua za ujenzi wake zimeshaanza.

Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumatatu Septemba 29, 2025 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
Amesema utekelezaji wa mradi huo wa soko la Samaki, utagharimu Sh1.3 bilioni na ndani yake kutakuwa na mtambo wa kukaushia dagaa.


