Wawekezaji Mkoani Manyara, wamemkaribisha kwa kishindo mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza baada ya kutua kwa Chopa inayohamasisha wananchi kumchagua Dkt. Samia, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, David Mulokozi amesema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia mazingira ya uwekezaji yameboreshwa zaidi nchini, hali iliyopelekea wawekezaji wa ndani na nje kuongezeka.

Dkt. Samia Suluhu Hassan, yupo Mkoani Manyara kwa ziara ya kampeni katika wilaya mbalimbali mpaka Oktoba 4,batakapomalizia kampeni zake katika viwanja vya stendi ya zamani ya Babati Mjini.


