Na Saulo Stephen – Singida.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt Fatma Mganga, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa mapato ya ndani pamoja na fedha kutoka Serikali Kuu.
Dkt Mganga alitoa pongezi hizo Juni 10, 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Miradi aliyotembelea na kujionea hatua za utekelezaji wake ni pamoja na ujenzi wa jengo la utawala katika Shule ya Sekondari Mungumaji na Unyianga, pamoja na maabara ya Shule ya Sekondari Kindai. Aidha, alitembelea ujenzi wa Shule ya Amali ya Mkoa wa Singida, nyumba ya walimu 2(1) katika Sekondari ya Utemini na jengo la wazazi katika Kituo cha Afya Sokoine.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri na matumizi mazuri ya mapato ya ndani. Ni muhimu kuendelea kusimamia miradi hii hadi ikamilike kwa viwango vilivyokusudiwa, sambamba na kutekeleza maelekezo.
