DKT. BAGANDA NA WENZAKE WANNE MAHAKAMANI KWA KESI YA FEDHA ZA UMITASHUMTA SINGIDA

Na Saulo Stephen – Singida.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Elipidius Baganda, pamoja na wenzake wanne, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Singida wakikabiliwa na tuhuma za utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 44.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Fadhil Luvinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Marshal Mseja, amesema kuwa fedha hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya shughuli za michezo za shule za msingi kupitia mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2023, lakini Dkt. Baganda anadaiwa kuzitumia kwa matumizi binafsi.

Washtakiwa wengine waliotajwa katika kesi hiyo ni: Evance Mlongo, mwalimu wa Shule ya Sekondari Mughanga, Paschal Kichambati mkuu wa shule ya sekondari ya Mghanga, James Lazaro Watatu wa mwisho ni watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na wanashtakiwa kwa kosa la kutoa msaada katika kutekeleza kosa hilo.

Kutokana na uzito wa mashtaka yanayomkabili, Dkt. Baganda amenyimwa dhamana na amepelekwa rumande.

Hali kama hiyo imemkumba pia mshatakiwa wa pili, Mwl. Evance Mlongo, ambaye ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Washtakiwa wengine watatu wamefanikiwa kupata dhamana, na kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Juni 18, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *