Mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia nchini Tanzania Dkt Wilbroad Slaa ameachiwa kwa dhamana masaa machache yaliyopita ikiwa ni siku chache baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa makosa ya uhaini.
Taarifa za kuachiliwa kwa Dk. Slaa zimekuja ndani ya masaa 24 baada ya jopo la mawakili wanaomtetea yeye na wenzake watatu kufungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwendesha Mashtaka Mkuu, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa Polisi Kituo Kikuu cha Mjini Mbeya kwa kuendelea kuwashikilia wateja wao kinyume na taratibu za kisheria.