DIWANI KATA YA SOLWA AFARIKI DUNIA

NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA   

Zikiwa zimesalia miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  October 2025 ,Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Awadh Hafiz amefariki dunia kwa ajali baada ya bajaji aliyokuwa akisafiria kugongwa na basi la kampuni ya Frester.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 19, 2025 wakati marehemu akiwa safarini kutoka eneo la Kolandoto kuelekea Shinyanga Mjini, ambapo bajaji aliyopanda iligongana na basi hilo, maeneo ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga  na kusababisha majeraha makubwa yaliyosabisha kifo chake.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni kamishina mwandamizi wa jeshi hilo SACP Janeth Magomi  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  ambapo amesema gari la abiria lilitaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari na kwenda kugonga bajaji hiyo  

Jambo media inatoa pole kwa wafiwa wote na mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *