Na Saulo Stephen-Singida.
Aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida na Diwani wa kata ya Majengo kwa kipindi cha 2020 – 2025 ,Bi Yagi Kiaratu leo Juni 28 amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Bi. Yagi Kiaratu amechukua fomu hiyo ya mbio za kuwania nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo Fomu hiyo ameichukua katika ofisi za chama hicho wilaya ya Singida Mjini.
Katika Kipindi chake cha Uongozi wa udiwani wa kata ya Majengo ,pamoja na nafasi ya Meya katika Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu anafahamika kwa kuwa Kiongozi mwanamama mwenye fikra pevu, maono ya maendeleo na moyo wa kizalendo kwa wananchi wa Singida Mjini.
Zoezi la uchukuaji fomu linaendelea katika ofisi za chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Mjini kwa hali ya utulivu na mshikamano, ambapo linatarajia kufika kikomo Julai 2 Mwaka huu 2025.