Diddy avunja ukimya tuhuma za ubakaji

Mkongwe wa muziki Diddy, amevunja ukimya kwa kuweka wazi amechoshwa na tuhuma zinazosambazwa juu yake kwa wiki kadhaa, ambapo kuliibuka Madai ya kufanya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake akiwemie EX-Wake (Cassie) na pia mwanamke mmoja ambaye anadai alibakwa 1991.

Diddy ameachia taarifa fupi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Kwa wiki kadhaa zilizopita, nimekaa kimya na kuangalia watu wakijaribu kuniua kwa sifa yangu, kuharibu sifa yangu na urithi wangu. Madai machungu yamefanywa dhidi yangu na watu binafsi wanaotafuta pesa haraka. Niruhusu niwe wazi kabisa: Sikufanya jambo baya lolote linalodaiwa.” 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *