Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Diddy ashtakiwa kwa ubakaji

Rapa Mkongwe na mtayarishaji wa muziki,  Sean Combs ‘Diddy’ amefunguliwa kesi ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono na aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Cassie.

Katika kesi hiyo, iliyowasilishwa katika Mahakama ya Manhattan, rapa huyo anadaiwa kufanya vitendo hivyo kwa takriban muongo mmoja.

Katika kesi hiyo, iliyowasilishwa na Cassie, ambaye jina lake halisi ni Casandra Ventura – anasema muda mfupi baada ya kukutana naye mwaka wa 2005, alipokuwa na umri wa miaka 19, alianza, mtindo wa kudhibiti na unyanyasaji ambao ulijumuisha kumtumia dawa za kulevya, kumpiga na kumlazimisha kufanya mapenzi na msururu wa makahaba wa kiume huku akirekodi matukio hayo.

Mnamo mwaka wa 2018, kesi hiyo inasema, karibu na mwisho wa uhusiano wao, Diddy alilazimisha kuingia nyumbani kwake na kumbaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *