DIARRA APIGWA ‘STOP’ MECHI TATU, SIMBA ADHABU MILIONI 10

“Screen Protector” Djigui Diarra ambaye ni mlinda mlango Young Africans amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Shilingi Milioni 2 kwa makosa ya utovu wa nidhamu kwenye mchezo dhidi yao na Mtibwa Sugar, uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeeleza kuwa adhabu hiyo inatokana na kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu, juu ya Udhibiti kwa Wachezaji.

Djigui Diarra.

Aidha, mchezaji huyo raia wa Mali, pia ametozwa faini ya Shilingi Milioni 2, kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Ktatika hatua nyingine, Klabu ya Soka ya Simba imetozwa faini ya Shilingi Milioni 10, kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa waamuzi mara baada ya mchezo kati yao na Pamba Jiji FC, uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *