Diamond Platnumz sio mmiliki wa ziiki

Kampuni ya Ziiki Media hivi karibuni ilikutana na waandishi wa habari ambapo iliweka sawa juu ya taarifa zilizozagaa kuwa msanii Diamond Platnumz ndiye mmiliki wa Kampuni hiyo ya Usambazaji wa Muziki ambapo Meneja wa kampuni hiyo, Camilla Owora alikanusha taarifa hizo.

Bi. Camilla alisema kuwa Ziiki Media haijawahi kuwa na ubia wa aina yoyote na Diamond zaidi ya kuingia naye mikataba ya kusambaza kazi zake na za wasanii waliopo chini ya lebo yake WCB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *