Staa wa muziki na CEO wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ameweka nadhiri ya kushiriki kwenye albamu mpya ya msanii wa Singeli nchini Sholo The Rock iitwayo ‘Another Boy from Tandale’.
Katika Podcast aliyofanya hivi karibuni Sholo amesema anafanya albamu hiyo kwa sababu alipata msukumo kutoka kwenye albamu ya Diamond iitwayo A Boy from Tandale, iliyotoka Machi 14,2028.
Baada ya hapo Diamond akaona post hiyo na kuandika ; “MWAMBA THE ROCK!… my homeboy Brother, Love always!..InshaAllah Lazma niwepo kwenye Album hio Mwanangu!…. ANOTHER BOY FROM TANDALE”.