
Mke wa Alikiba, Aminah kupitia wanasheria wake mnamo Agosti 10, 2023 kutoka kampuni ya Shabaan Associaties LLP, walimuandikia barua ya kumtaka msanii wa muziki Diamond Platnumz kumuomba radhi mteja wao kufuatia tuhuma alizozitoa kipindi cha hivi karibuni katika mitandao ya kijamii.
Ambapo walimpa siku saba za kufanya hivyo na kumtaka kutumia mitandao wake wa kijamii kuandika ujumbe wa kuomba radhi.