Diamond Platnumz akutana naRais Kagame

Usiku wa jana Rais wa Rwanda, Paul Kageme alikutana na staa wa muziki Bongo Diamond Platnumz ambaye alifanya shoo kwenye Giants of Africa Festival nchini humo, ambapo wasanii kama Davido na Tiwa pia watafanya shoo siku zijazo.

Tamasha hilo pia linahusisha Tamasha la Mpira wa Kikapu la Vijana la ‘Giants of Africa’ litaandaliwa mjini Kigali, Rwanda kuanzia Agosti 13 hadi 19 mwaka huu. Vijana wapato 250 watapiga kambi BK Arena mjini Kigali kwa ajili ya mchezo wa mpira wa kikapu, elimu na utamaduni.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki tamasha hilo, ikiwemo Kenya, Nigeria, Burkina Faso, Ivory Coast, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Somalia, Uganda, Botswana, Ghana, Sudan Kusini, Morocco, Cameroon na Mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *