Staa wa muziki wa Bongo Diamond Platnumz ameshare ushindi wake wa tuzo zake tatu (hat-trick) za Magic Vibe Awards zilizotolewa wikiendi iliyopita.
Pia hivi karibuni msanii wa muziki Harmonize aliibuka na tuzo tatu AEAUSA, ambazo alizipata kutoka nchini Marekani.
Hii ni mara ya tatu Diamond Platnumz kushinda tuzo tatu, kwani mwaka 2015 kwenye tuzo za All Africa music awards AFRIMA zinazotolewa nchini Nigeria alishinda ,pia tuzo za African Music magazin awards AFRIMMA 2015 alishinda tuzo tatu.