Usafirishaji haramu wa dhahabu nje ya Afrika hasa kuelekea katika Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) umeongezeka katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Uchambuzi uliofanywa na Swissaid, umegundua kuwa jumla ya tani 435 za dhahabu, inayochimbwa zaidi na wachimbaji migodi wadogo na yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 30, ilisafirishwa nje ya Afrika mnamo mwaka 2022.
Usafirishaji haramu wa dhahabu kutoka Afrika umeelezwa katika ripoti iliyochapishwa leo na shirika la Swissaid, linaloangazia misaada ya maendeleo na uhamasishaji
Uchambuzi uliofanywa na Swissaid, umegundua kuwa jumla ya tani 435 za dhahabu, inayochimbwa zaidi na wachimbaji migodi wadogo na yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 30, ilisafirishwa nje ya Afrika mnamo mwaka 2022.
Swissaid imesema UAE ndio kituo kikuu cha dhahabu hiyo kutoka Afrika na kwamba muongo mmoja awali, ilipokea zaidi ya tani 2,500 za dhahabu yenye thamani ya jumla ya zaidi ya dola bilioni 115.