Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Philipo Mhina mkazi wa Nyasaka jijini Mwanza kwa kosa la kumgonga askari wa kitengo cha usalama barabarani na kusababisha kifo chake.
Akielezea tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni dereva wa gari la Shule ya Msingi Nyamuge alisimamishwa na askari huyo kwa ajili ya ukaguzi ila baada ya gari hiyo kukutwa na kosa alimtaka dereva huyo arudishe nyuma gari kwa ajili ya usalama ndipo alipomgonga askari huyo na kusababisha kifo chake.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewataka madereva kuendelea kuchukua tahadhari, kufuata sheria za usalama barabarani pamoja na kujali usalama kwa watumiaji wengine wa barabara ili kuepusha madhara ambayo yanayoweza kuepukika.