Wababe kutoka Minneapolis Minnesota, Minnesota Timberwolves imewatupa nje mabingwa watetezi wa NBA Denver Nuggets, kwa kuwachapa vikapu 98-90 katika mchezo wa 7 wa maamuzi wa nusu fainali ya kanda ya Magharibi.
Wakali Karl Anthony Towns na Jaden McDaniels kila mmoja amepiga pointi 23 katika ushindi huo wa Minnesota ambao watacheza fainali ya kanda ya Magharibi dhidi ya Dallas Mavericks, mchezo wa kwanza utapigwa alfajiri ya alhamisi.
Nao Indiana Pacers wametinga fainali ya kanda ya mashariki kwa ushindi wa vikapu 130-109 dhidi ya New York Knicks, ambapo sasa watacheza fainali dhidi ya Boston Celtics, mchezo wa kwanza utapigwa alfajiri ya jumatano.