DENI LA TAIFA ZANZIBAR LAPANDA KWA ASILIMIA 208, HAYA NI MANENO YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS.

DENI LA ZNZ LAFIKIA TRION 2 Bilioni 397 -RIKA LOTE ZNZ WATALILIPA

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman amewataka Wazanzibar kushughulikia deni kubwa la Umma ambalo amedai limepanda kwa asilimia 208.

Othman ameyasema hayo wakati akihutubia mbele ya wahariri na wanahabari ambapo amesema Deni la Umma la Zanzibar limetoka Bilioni 887 Hadi Tsh Trilioni 2 na Bilioni 397 ambapo amesema kwa kila mzanzibar wa rika lolote pamoja na watoto wachanga wanaonyonya wanadeni la shilingi laki moja na elfu kumi na tisa mia nane hamsini (119,850) ambalo watapaswa kulipia.

Mh. Othman amesema fedha hizo zinadaiwa na wakopeshaji wa kimataifa bila ya kuingiza madeni ya ndani huku akidai zipo baadhi ya fedha zimehamishiwa akaunti za nje na kwamba swali hilo linawezekana kushughulikiwa

” Kama Mkurugenzi wa Mashtaka wa zamani na mwanasheria Mkuu wa Serikali naweza kuwahakikishia kwamba hilo ni jambo linalowezekana hasa na kutokana na mfumo wa sasa wa kusimamia sheria kwa makosa ya namna hiyo’. Othman Makamo wa Kwanza Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *