Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais (Tamisemi), imeeleza kuwa Waziri wa wizara hiyo, Mohamed Mchengerwa amefikia uamuzi huo baada ya Mbenje kushindwa kutimiza majukumu yake, hivyo amewekwa pembeni ili kupisha uchunguzi

Mchengerwa amesema katika taarifa hiyo kwamba Mbenje amelegalega katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kutokana na hatua hiyo, Mchengerwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi, Adolf Ndunguru kutuma timu ya uchunguzi katika halmashauri hiyo.
Dalili za kusimamishwa kwa Mbenje zilionekana mapema
katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo, ambapo Makonda alieleza kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkurugenzi huyo naayelalamikiwa na wananchi wa halmashauri hiyo.


