Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

DCI yakanusha kumkamata Davido akiwa na dawa za kulevya

Ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya (DCI), imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni na kuchapishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba mwimbaji staa wa Nigeria Davido amekamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Nairobi Kenya akituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya.

Mapema siku ya leo baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya na nchi jirani ikiwemo Tanzania vilichapisha habari iliyodai Davido ambaye alikuwa nchini Kenya kwa kazi zake za sanaa, amekutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine kwenye ndege yake binafsi zenye thamani ya shilingi za Kenya milioni 18 na kuzuiliwa asiondoke kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *